Chama mchezaji bora mwezi Aprili

Kiungo mshambuliaji, Clatous Chama amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi wa Aprili (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Chama raia wa Zambia amewashinda mlinda mlango Aishi Manula na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe ambao aliingia nao fainali.

Tuzo hii inadhaminiwa na Emirate Aluminium Profile hushindanisha nyota watano waliofanya vizuri zaidi kabla ya kuchujwa hadi watatu na Kamati maalumu na kupigiwa kura na mashabiki hadi mshindi apatikane.

Chama anakuwa mchezaji wa tatu kuchukua tuzo hiyo tangu ilipoanza kutolewa Februari baada ya Luis Miquissone na Joash Onyango.

Huu hapa mchanganuo wa kura zilivyopigwa:

Clatous Chama – 50.48%

Aishi Manula – 30.74%

Shomari Kapombe – 18.78%

Leave a comment