Baada ya majadiliano na Uongozi kumalizika vizuri kiungo mshambuliaji Clatous Chama ataondoka nchini muda wowote kutoka sasa kuelekea Uturuki kujiunga na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya msimu.
Chama ataondoka pamoja na kiungo mkabaji, Fabrice Ngoma ambaye mchakato wa kupata vibali vya kuingia Uturuki unaendelea vizuri.
Wawili hao wakifika Uturuki itakuwa wachezaji wote tuliowasajili kwa ajili ya msimu ujao watakuwa wamekamilika ukicha ambao bado hatujawatangaza.
Programu ya mazoezi zinaendelea vizuri ambapo kwa sasa wachezaji wanafanya asubuhi na jioni.