Chama, Kapama wasimamishwa

Uongozi wa klabu umewasimamisha wachezaji wawili viungo, Clautos Chama na Nassor Kapama kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Kufuatia vitendo hivyo wachezaji hao watapelekwa katika kamati ya nidhamu kwa hatua zaidi za kinidhamu.

Simba imekuwa na utaratibu wa kuwapeleka kamati ya nidhamu wachezaji ili nao wao wapewe nafasi ya kusikilizwa kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi yao.

Uongozi unapenda kuwakumbusha watumishi wake kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu kwani klabu haitasita kumchukulia hatua yeyote atakayethibitika kwenda kinyume na utaratibu huo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER