Chama awashukuru wachezaji, mashabiki tuzo ya Agosti

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama amewashukuru wachezaji wenzake na mashabiki waliosababisha kuchaguliwa mchezaji bora wa mwezi Agosti (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Chama amesema tuzo hiyo kwa nje inaonekana kama binafsi lakini inatokana na ushirikiano mkubwa aliopata kutoka kwa wachezaji wenzake na mashabiki waliompigia kura.

Chama anakuwa mchezaji wa kwanza kushinda tuzo hiyo msimu huu baada ya kuwapiku Sadio Kanoute na Pape Sakho.

“Naishukuru familia yangu, wachezaji wenzangu na mashabiki kwa kunisaidia kushinda tuzo hii, bila wao nisingeweza ingawa inaonekana kama binafsi. Tuzo hii inaongeza morali kwa timu ukingatia huu ni mwanzo wa msimu,” amesema Chama.

Kwa upande wake Ofisa Mahusiano wa Emirate Aluminium Profile, Issa Maeda amesema wanaendelea kutoa bidhaa mpya zenye ubora mkubwa ili kuendana na hali halisi inavyotaka.

Kwa kuibuka mshindi Chama amekabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER