Chama arejea Manula, Taddeo kuikosa Mbeya City kesho

Kiungo wetu mshambuliaji, Clatous Chama amerejea kikosini kutoka nchini kwao Zambia baada ya kumaliza mazishi ya mke wake aliyefariki mwanzoni mwa mwezi huu.

Baada ya kurejea Chama amejiunga moja kwa moja kambini ambapo leo asubuhi amefanya mazoezi na wenzake kujiandaa na mchezo wa kesho wa ligi dhidi ya Mbeya City.

Wakati Chama akirejea kikosini kesho tutakosa huduma ya mlinda mlango wetu Aishi Manula na kiungo Taddeo Lwanga ambao wanatumikia adhabu ya kadi tatu za njano.

Kocha msaidizi, Seleman Matola amesema baada ya kikosi kurejea jana kutoka jijini Mwanza kilipocheza mechi dhidi ya Polisi Tanzania kiliingia kambini moja kwa moja kujiandaa na mechi ya kesho.

Matola amesema mchezo utakuwa mgumu kwa kuwa Mbeya City hawapo kwenye nafasi nzuri katika msimamo lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda ili kuzidi kusogelea ubingwa wa ligi kuu.

“Kikosi kiliingia kambini jana baada ya kurejea kutoka Mwanza kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa kesho na tunafurahi kiungo Clatous Chama amewasili na amejiunga na wenzake.

“Manula na Taddeo wao watakosekana kwenye mchezo wa kesho sababu wana kadi tatu za njano wakati Ibrahim Ajibu ni mgonjwa anasumbuliwa na malaria lakini wachezaji wengine wote wako fiti tayari kwa mechi,” amesema Matola.

SHARE :
Facebook
Twitter

6 Responses

  1. Habari njema kwa urejeo wa chama japo tutawakosa thadeo na manula,lakini naamini tuna kikosi kizuri chenye uwezo wa kucheza mechi yoyote,Kila la heri kwa Wanajeshi wetu,Aluta Continua

    1. Dah Manula juzi kaitafuta kadi ya njano hivi hivi.. kuchelewa kupiga free kick.. ila sio mbaya Kako time now atoe kutu.. all the best Simba

  2. Mbali na hvyo lakin zetu oint tatu Kwan ndio muhimu nje na hapo team/uongozi/mashabiki tuombe mungu tupate ushindi tu

  3. ni habari njema kusikia chama amerejea kwenye timu na amefanya mazoezi .lakini kuhusu manula na lwanga ninaamini simba inawachezaji wenye uwezo wa kuziba hizo namba hivo leo naitakia timu yangu ushindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER