Chama apiga hat trick tukiipiga ‘wiki’ Ruvu Shooting

Kiungo mshambuliaji Clatous Chama, amefunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa hatua ya 16 bora ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Nahodha John Bocco alitupatia bao la mapema dakika ya kwanza kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa kiufundi na Yusuf Mhilu.

Clatous Chama alitupatia bao la pili dakika ya 25 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Peter Banda kabla ya kumlamba chenga Renatus Ambrose chenga.

Dakika mbili baadaye Chama tena alitupatia bao la tatu akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi ya Mzamiru Yassin.

Bocco alitufungia bao la nne dakika ya 40 kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Gadiel Michael.

Ikiwa imesalia dakika moja kwenda mapumziko mlinzi wa Ruvu, Michael Masinda alijifunga na kutupatia bao la tano katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na Gadiel.

Muda mfupi baada ya kuingia kutoka benchi Jimmyson Mwinuke alitupatia bao la sita dakika 70 baada ya kupokea pasi kutoka kwa Chama akiwa ndani ya 18.

Chama alitupatia bao la saba dakika ya 73 akikamilisha hat trick yake baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Israel Patrick.

Kocha Pablo Franco aliwatoa Henock Inonga, Kapombe, Aishi Manula, Bocco na Banda na kuwaingiza Erasto Nyoni, Israel, Ally Salim, Bernard Morrison na Mwinuke.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER