Chama akabidhiwa tuzo yake ya mwezi Aprili

Kiungo mshambuliaji, Clatous Chama leo amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Aprili (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).

Chama amekabidhiwa tuzo hiyo katika Viwanja vya Mo Simba Arena na Wadhamini Emirate Aluminium Profile, kabla ya kuanza mazoezi ya jioni.

Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Chama amewashukuru wadhamini, wachezaji pamoja na mashabiki ambao wamempigia kura na kufanikisha jambo hilo.

“Ni heshima kubwa kwangu kupata tuzo hii, kwanza nawashukuru wadhamini kwa kuandaa sababu inaongeza thamani kwetu, pili nawashukuru wachezaji wenzangu kwa ushirikano wanaonipa uwanjani na mashabiki walionipigia kura,” amesema Chama.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Emirate Aluminium Profile, Issa Maeda amesema Kampuni hiyo inaridhishwa na utaratibu wa kumpata mshindi wa kila mwezi Kwa kua upo huru na wazi.

Chama amepata asilimia 50 ya kura zilizopigwa na kuwapiku mlinda mlango Aishi Manula na mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER