CEO Kajula aweka wazi mipango ya Utendaji wake

 

Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula ameweka wazi mipango ya Utendaji wake mbele ya wanachama katika Mkutano Mkuu baada ya kupewa jukumu hilo katikati ya juma hili.

Kajula amesema jambo la kwanza atakalofanya ni kuhakikisha anaiunganisha klabu kuanzia Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti, Wanachama mpaka mashabiki.

Katika siku yake ya kwanza ofisini ambayo itakuwa kesho Jumatatu, Januari 30 Kajula amepanga kwenda kuwatembelea wadhamini wetu.

Kajula amesema miongoni mwa vitu atakavyo visimamia ni:

­čö╣ Kuhakikisha wakati mwingine tutafanya Mkutano Mkuu wa kitkenolojia utakaowahusisha wanachama wote nchi nzima.

­čö╣Tutajenga timu imara kwa ajili ya mataji. Kuboresha benchi la Ufundi.

­čö╣Tutaimarisha brand ya klabu yetu na kuitumia vizuri kutuongezea kipato.

­čö╣Kusimamia ujenzi Hosteli za kisasa na tayari mchoro umekamilika.

­čö╣Kuboresha Sherehe za Simba Day

­čö╣Kuunganisha matawi kote nchi nzima

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER