CEO Kajula akabidhi Begi la jezi kwa mashujaa

Mtendaji Mkuu wa klabu, Imani Kajula amekabidhi begi la jezi kwa mashujaa ambao tayari kwa kuanza safari ya kulipeleka juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya uzinduzi rasmi siku ya Ijumaa.

Kajula amekabidhi begi hilo katika Kituo cha Mandara ambapo ndio cha kwanza vikibaki vingine sita kabla ya kufika kileleni.

Kajula amesema amewashukuru Waandishi wa Habari kwa kulitangaza kwa ukubwa suala hilo na kulifanya kuwa gumzo ndani na nje ya nchi.

“Tumefanikiwa kuwakabidhi bendera mashujaa wetu ambao watalipeleka begi kileleni mlima, hili ni jambo kubwa kwetu Simba.

“Tunavishukuru Vyombo vya Habari kwa kulibeba jambo hili na kulifanya kuwa kubwa zaidi. Simba inathamini sana mchango wenu na bado tunawahitaji,” amesema Kajula.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER