Cambiaso yatepeta mechi yetu ya kirafiki

Kikosi chetu kimeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Cambiasso katika mchezo wa kirafiki wa kimazoezi uliofanyika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena.

Wachezaji walioanza katika kikosi cha kwanza ni wale ambao hawakucheza au waliopata dakika chache katika mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya RS Berkane uliofanyika juzi Jumapili.

Mchezo ulianza kwa kasi ambapo iliwachukua dakika 10 wageni Cambiasso kupata bao baada ya walinzi wetu kuchelewa kuondoa hatari.

Erasto alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 19 baada ya kumalizia pasi ya Clatous Chama kufuatia Bernard Morrison kuanzisha kona fupi.

Kipindi cha pili Chama alitupatia bao la pili akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Yusuf Mhilu ambaye aliwazidi kasi walinzi wa Cambiaso.

Kikosi chetu kilivyopangwa

Beno Kakolanya (30),Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Pascal Wawa (6), Kenedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Bernard Morrison (3), Taddeo Lwanga (4), Chris Mugalu (7), Clatous Chama (17), Jimmyson Mwanuke (21).

Kocha Pablo Franco aliwatoa Jimmyson, Erasto, Morrison na kuwaingiza Peter Banda, Mzamiru Yassin, Yusuf Mhilu

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER