Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeruhusu idadi ya mashabiki 35,000 katika mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendarmerie utakaopigwa Aprili 3.
Ingawa tulitamani kuongeza idadi ya mashabiki zaidi ya tuliyopata kutokana na umuhimu wa mechi yenyewe lakini CAF imekubali kuruhusu idadi hiyo ya siku zote.
Tayari tiketi zimeanza kuuzwa leo kwa njia ya mitandao ya simu ikiwa bado siku tisa kabla ya mchezo ili kuwafanya mashabiki wanunue mapema.
Uongozi unahamasisha mashabiki kununua tiketi mapema ili kuepusha usumbufu siku ya mchezo.
One Response