Kiungo mshambuliaji Rally Bwalya, amesema baada ya kukosa nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa sasa ni wakati wa kufanya hivyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Kiungo huyo Mzambia ameweka wazi kuwa malengo ya wachezaji pamoja na benchi la ufundi ni kuhakikisha tunaingia makundi kwa kuitoa Red Arrows.
Bwalya amesema mchezo wetu wa kwanza dhidi Wazambia hao utakuwa mgumu kwa sababu wapinzani nao watataka kutafuta matokeo ugenini ili kurahisisha mechi ya marudiano lakini tuko tayari kuwakabili katika mechi zote mbili.
“Red Arrows si timu mbaya ndiyo maana imefika hatua hii na hatutaidharau, tutaingia uwanjani kupambana kutafuta ushindi tukijua tupo nyumbani. Tutaingia uwanjani kuhakikisha tunapambana kutafuta ushindi.
“Tulikuwa na nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa lakini ikashindikana, sasa tumepata tena nafasi ya kufanya hivyo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika tutahakikisha inawezekana,” amesema Bwalya.
One Response