Bwalya afunguka staili yake ya kushangilia

Kiungo wetu mshambuliaji Rally Bwalya, amesema aina yake ya ushangiliaji anapofunga bao huwa anamaanisha licha ya kupitia magumu lakini kuna mwanga na baraka mbele yake.

Bwalya raia wa Zambia amesema timu inapitia kipindi kigumu hivyo aina yake ya ushangiliaji inarejesha morali baina ya wachezaji na mashabiki.

“Maana ya staili yangu ya ushangiliaji ni haijalishi shida tunayopitia lakini kuna baraka na mwanga mwishoni mwa safari,” amesema Bwalya.

Bwalya amehusika katika mabao manne kwenye mechi zetu tatu zilizopita huku akiendelea kuonyesha kiwango bora kila mchezo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER