Bodi yakutana kujadili mipango ya klabu

Bodi ya Wakurugenzi chini ya Mwenyekiti Salim Abdallah ‘Try Again’ leo imekutana jijini Dar es Salaam na kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya klabu.

Miongoni mwa vitu vilivyojadiliwa ni mpango mkakati wa kuhakikisha timu inaendelea kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu ya NBC, maandalizi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itaanza Februari mwaka 2023.

Pia maandalizi ya michuano ya Azam Sports Federation (ASFC) ambayo taji lake tulilipoteza msimu uliopita na tunahitaji kulirejesha.

Bodi pia imejadili mipango ya timu ya Simba Queens kuelekea kuanza kwa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) Desemba 6 ambayo sisi ni mabingwa watetezi.

Mbali na masuala ya timu pia Bodi imejadili kuhusu maendeleo ya ujenzi wetu wa Uwanja wa Mo Simba Arena ambao utaingia hatua ya pili wakati ujenzi wa uzio ukiwa mbioni kukamilika.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER