Bocco: Tunawashukuru mashabiki wetu kwa sapoti kubwa

Nahodha, John Bocco amewashukuru mashabiki wetu kujitoa kwa ajili timu katika nyakati zote hali inayowafanya wachezaji kujiona wana thamani kubwa ndani ya kikosi.

Bocco amesema mashabiki wetu wamekuwa pamoja na timu katika nyakati zote bila kujali matokeo gani yamepatikana.

“Kwa niaba ya wachezaji nawashukuru mashabiki wetu kwakuwa nasi siku zote katika mazingira yote. Iwe furaha au huzuni wapo pamoja nasi.”

“Tumetoka kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini wamekuja kwa wingi Uwanja wa Ndege kuja kutupokea, tuna uthamini mchango wao na tumejipanga kuwalipa furaha wakati mwingine,” amesema Bocco.

Akizungumzia michuano ya Ligi ya Mabingwa, Bocco amesema tunaendelea kujifunza kila wakati ili wakati mwingine tufanye vizuri zaidi.

“Miaka ya nyuma ilikuwa tukifikia hatua ya makundi ni mafanikio, sasa tunaweza kufika robo fainali bila wasi wasi, tunaamini tutaweza kufika mbali zaidi kipindi kijacho,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER