Bocco, Phiri wang’ara Malawi

Mabao mawili yaliyofungwa na washambuliaji Moses Phiri na John Bocco yametuwezesha kuibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Nyasa Big Bullets katika mchezo wa hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa Uwanja wa Bingu Mutharika nchini Malawi.

Mabao hayo ambayo yamefungwa kila kipindi yametuweka kwenye nafasi nzuri ya kutinga hatua ya kwanza ya michuano hiyo.

Phiri alitupatia bao la kwanza dakika ya 30 kwa mpira wa ‘acrobatic’ akiwa ndani ya 18 baada ya kumlaizia pasi ya kichwa ya Kibu Denis kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa na Clatous Chama.

Baada ya bao hilo tuliendelea kumiliki mchezo na kupiga pasi fupi fupi ambapo tuliifanya mechi kuwa ya taratibu.

Nahodha Bocco alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la pili dakika ya 84 baada ya Chama kuwalamba chenga walinzi wa Bullets kabla ya kutoa pasi.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Phiri, Sadio Kanoute, Pape Sakho na Kibu na kuwaingiza Bocco, Peter Banda, Erasto Nyoni na Augustine Okrah.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER