Nahodha John Bocco ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu (MVP) msimu wa 2020/21 katika hafla ya utoaji tuzo iliyofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), jijini Dar es Salaam.
Bocco amewashinda aliyekuwa kiungo wetu mshambuliaji Clatous Chama na kiungo Mukoko Tonombe wa Yanga aliokuwa ameingia nao kwenye fainali ya kinyang’anyiro hicho.
Hii ni mara ya pili Bocco kushinda Tuzo ya MVP akiwa ndani ya kikosi cha Simba baada ya kufanya hivyo mwaka 2018 alipowashinda Emmanuel Okwi na Erasto Nyoni.
Bocco pia ameshinda Tuzo ya mfungaji bora ambapo alimaliza na mabao 16 huku akitajwa kwenye kikosi bora cha msimu.