Bocco, Mugalu kuongoza mashambulizi dhidi ya Kaizer

Kocha Didier Gomes amefanya mabadiliko kidogo ya kikosi kuelekea mchezo wa leo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs ambapo ameanza na washambuluaji wawili John Bocco na Chris Mugalu.

Mara nyingi Gomes amekuwa akiamini katika matumizi ya mshambuliaji mmoja na viungo watatu wa ushambuliaji lakini kutokana na asili ya mchezo kuhitaji idadi kubwa ya mabao ameamua kuanza na mawili.

Tunapaswa kupindua matokeo kwa kufunga mabao matano ili kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ndiyo sababu Gomes amewaanzisha pamoja Bocco na Mugalu.

Mabadiliko mengine aliyofanya Gomes ni kumuanzisha Mzamiru Yassin katika kiungo wa ulinzi sambamba na Taddeo Lwanga akichukua nafasi ya Jonas Mkude ambaye alicheza mchezo wa kwanza kule Johannesburg.

Kikosi kamili: Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16)
Pascal Wawa (6), Taddeo Lwanga (4), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Chris Mugalu (7), Luis Miquissone (11).

Wachezaji wa Akiba: Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Said Ndemla (13), Bernard Morrison (3), Miraji Athumani (21), Medie Kagere (14), Rally Bwalya (8) Francis Kahata (25).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER