Bocco mchezaji bora wa wiki Afrika

Nahodha John Bocco ameibuka mchezaji bora wa wiki wa Ligi ya Mabingwa Afrika katika ya  hatua ya Robo Fainali.

Bocco ameibuka kidedea baada ya kuonyesha kiwango safi kwenye mchezo wetu dhidi ya Kaizer Chiefs tulioibuka na ushindi wa mabao 3-0 Jumamosi iliyopita ambapo alifunga mawili.

Nahodha wetu huyo ameibuka kidedea baada ya kuwashinda nyota watatu Farouk Ben Mustapha wa ES Tunis, Wahid El Karti wa Waydad Casablanca na Mosa Lebusa wa Mamelodi Sundowns.

Mchanganuo wa kura zilizopigwa.

John Bocco 83%

Mosa Lebusa 8%

Wahid El Karti 5%

Farouk Mustapha 5%

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER