Bocco mchezaji bora mwezi Mei

Nahodha John Bocco ameibuka kidedea kwenye kinyang’anyiro cha Mchezaji Bora wa Mwezi wa Mashabiki (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month) baada ya kupata kura nyingi.

Bocco amewashinda kiungo mshambuliaji Bernard Morrison na kiungo mkabaji Taddeo Lwanga ambao waliingia fainali kwenye kinyan’ganyiro hicho.

Tuzo hiyo inadhaminiwa na Kampuni ya Emirate Aluminium Profile ambapo wachezaji watatu huingia fainali na kupigiwa kura na mashabiki kupitia tovuti hii ya klabu.

Bocco atakabidhiwa kitita cha Sh 1,000,000 na Emirate Aluminium kama zawadi ya ushindi.

Mchanganuo wa kura zilivyopigwa:

John Bocco – 3, 942 (59.3%)

Bernard Morisson – 1,956 (29.4%)

Taddeo Lwanga kura 744 (11.3%)

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER