Bocco kuongoza mashambulizi dhidi ya Kagera

Nahodha John Bocco amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Kagera Sugar utakaopigiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku.

Bocco ambaye alikuwa majeruhi na katika mechi kadhaa zilizopita amekuwa akiingia kutoka benchi lakini leo Kocha Pablo Franco na benchi lake wameamua kumuanzisha.

Katika mchezo uliopita dhidi ya Ruvu Shooting, Bocco alitokea benchi na kufunga bao la tatu katika ushindi wa mabao 4-1.

Mlinzi wa kati Henock Inonga leo amepangwa kama kiungo mkabaji sambamba na Mzamiru Yassin kutokana na wachezaji watatu wa eneo hilo kuwa majeruhi.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Pascal Wawa (6), Henock Inonga (29), Pape Sakho (10), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Rally Bwalya (8), Kibu Denis (38).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Peter Banda (11), Medie Kagere (14), Yusuf Mhilu (27), Jimmyson Mwanuke (21).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER