Nahodha John Bocco na kinara wa ufungaji Medie Kagere wataongoza safu ya ushambuliaji kwenye mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Gwambina FC utakaopigwa kwenye Uwanja wa Gwambina Complex uliopo Misungwi jijini Mwanza.
Mara kadhaa Kocha Didier Gomez amekuwa akitumia mshambuliaji mmoja na kuweka viungo watatu wa ushambuliaji lakini leo amekuja tofauti na kuwaanzisha Bocco na Kagere.
Hadi sasa Kagere ana mabao 11 na ndiye kinara wa ufungaji kwenye ligi akifuatiwa na Bocco mwenye mabai 10.
Kiungo mshambuliaji Bernard Morrison naye ameanza akichukua nafasi ya Luis Miquissone anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
Kikosi kamili kilivyopangwa
1. Aishi Manula
2. Shomari Kapombe
3. Mohamed Hussein
4. Kennedy Juma
5. Joash Onyango
6. Erasto Nyoni
7. Clatous Chama
8. Mzamiru Yassin
9. Medie Kagere
10. John Bocco ©
11. Bernard Morrison
Wachezaji wa Akiba
Gk.. Beno Kakolanya
02. Gadiel Michael
03. Ibrahim Ame
04. Jonas Mkude
05. Rally Bwalya
06. Chris Mugalu
07. Hassan Dilunga
One Response
Jambo jemaa