Baada ya kufunga mabao matatu ‘hat trick’ kwenye ushindi 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting jana, Nahodha John Bocco amesema kitu cha kwanza ni kuisaidia timu kupata ushindi mengine yanafuata.
Bocco amesema kufunga mabao matatu ni jambo zuri lakini yeye anaangalia zaidi kuisaidia timu kupata ushindi na kuwapa furaha mashabiki.
Nahodha Bocco amesema lengo ni kuhakikisha anatumia vizuri kila nafasi anayoipata uwanjani ili kuifanya timu kupata ushindi.
“Jambo la kwanza ni kuisaidia timu kupata ushindi halafu mengine yanakuja kama ziada. Kufunga hat trick ni jambo jema ila timu kwanza,” amesema Bocco.
Kwa muda mrefu Bocco amekuwa nje ya uwanja akiuguza majeraha na jana ndiyo amerejea na kufunga hat trick.