Bocco: Hatutabweteka na rekodi za kwa Mkapa

Nahodha John Bocco, amesema hatupaswi licha ya kuwa na rekodi nzuri tunapokuwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa hasa kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika hawapaswi kuliangalia hilo katika mechi ya kesho dhidi ya AS Vita.

Amesema badala yake kikosi kimejipanga kupambana ndani ya dakika 90.

Bocco amesema mara ya mwisho tulipokutana kwenye uwanja huo mwaka juzi tulifanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-1 hivyo hatupaswi kuamini itakuwa rahisi kupata ushindi bila kupambana.

Nahodha huyo ameongeza kuwa wachezaji wote wapo tayari na kila atakayepata nafasi atahakikisha anaitumia vema ili kujihakikishia ushindi unapatikana.

“Tunafahamu tuna rekodi nzuri tukiwa Uwanja wa Benjamin Mkapa lakini haituhakikishii kupata ushindi kesho, tunapaswa kupambana kucheza dakika 90,” amesema Bocco.

Matokeo ya ushindi au sare ya aina yoyote itatufanya kutinga moja kwa moja kwenye hatua ya robo fainali ya michuano hii.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER