Bocco: Hatuna presha ya kurejea kileleni

Nahodha wa timu John Bocco, amesema hatuna presha ya kurejea kileleni mwa msimamo ingawa amekiri ligi ya msimu huu ni ngumu.

Bocco amesema timu yetu inapambana kuhakikisha tunarudi kileleni mwa msimamo licha ya ugumu huo ambapo kila kitu kinaenda sawa na malengo hayo yatafikiwa hivi karibuni.

Bocco amesema hayo akizungumzia mchezo wetu ujao wa ligi dhidi ya Azam FC utakaopigwa Januari mosi Uwanja wa Benjamin Mkapa kuongeza kuwa utakuwa mgumu lakini tutahakikisha tunapata ushindi.

“Azam ni timu bora tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini kwa maandalizi tunayofanya tunaamini tutaibuka na ushindi. Tunawaheshimu Azam lakini tutafuata maelekezo tutakayopewa na mwalimu na tunaamini tutafanikiwa,” amesema Bocco.

Kuhusu Kombe la Shirikisho na timu yetu kupangwa kundi D pamoja na timu za RS Berkane, Asec Mimosas na US Gendamarie kwenye hatua ya makundi, Bocco amesema si kundi rahisi na tunapaswa kujiandaa vya kutosha.

“Ni kundi gumu na kila hatua ya michuano ya Afrika inakuwa ngumu ila tutapambana katika kila mchezo kuhakikisha tunafanya vizuri na kutimiza malengo tuliyojiwekea,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER