Bocco: Hatuna presha na ASEC

Pamoja na ubora na uzoefu wa wapinzani wetu ASEC Mimosas kwenye michuano ya Afrika Nahodha John Bocco amesema hatutaingia uwanjani kesho kwa presha wala kuwaogopa.

Bocco amesema tunawaheshimu ASEC ni timu nzuri na historia kubwa Afrika lakini hatuna presha kwa kuwa tuko nyumbani na tumejipanga kushinda.

Bocco amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kuwapa sapoti wachezaji ambapo ameahidi kuwapa furaha.

“Tunaiheshimu ASEC ni timu bora na ina wachezaji wazuri lakini hatuigopi wala hatutaingia kwa presha. Tumejiandaa vizuri kimwili na kiakili kuhakikisha tunaibuka na ushindi.

“Kikubwa nawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi uwanjani kuja kutupa sapoti, tunaamini tutawapa furaha kwa kupata ushindi,” amesema Bocco.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER