Bocco asaini miaka miwili kusalia Simba

Nahodha John Bocco amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kusalia katika timu yetu utakaomuweka  hadi mwaka 2023.

Mkataba wa Bocco ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu lakini kutokana na uwezo na umuhimu wake uongozi umeamua kumuongeza kandarasi mpya mapema.

Bocco alijiunga nasi akitokea Azam FC msimu wa 2017/18 na tangu wakati huo tumetwaa ubingwa wa Ligi Kuu mara tatu mfululizo huku tukielekea kuchukua mara ya nne.

Ukiachilia mbali uwezo anaouonyesha uwanjani sifa nyingine aliyo nayo ni nidhamu lakini pia ni mfano wa kuigwa ndani ya kikosi.

SHARE :
Facebook
Twitter

5 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER