Bocco arejea na ‘Hat trick’ dhidi ya Ruvu

Nahodha John Bocco amefunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi wa 4-0 tuliyopata dhidi ya Ruvu Shooting kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Bocco alitupatia bao la kwanza dakika ya tatu baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Mohamed Hussein.

Dakika ya 17 Bocco alitupatia bao la pili baada ya kumalizia pasi ya Clatous Chama kufuatia shambulizi lililoanzia kwa mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.

Kapombe alitupatia bao la tatu dakika ya 36 baada ya kumzidi ujanja mlinzi mmoja wa Ruvu akimalizia pasi safi kutoka kwa Chama.

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 37 baada ya kuumizwa nafasi yake ikachukuliwa na Victor Akpan.

Bocco alitupatia bao la nne na kukamilisha hat trick yake dakika ya 70 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Henock Inonga, Bocco, Joash Onyango na Mzamiru na kuwaingiza Mohamed Ouattara, Kennedy Juma, Kibu Denis na Nassor Kapama.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER