Nahodha John Bocco leo amekabidhiwa tuzo yake ya Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Mei (Emirate Aluminium Simba Fans Player Of The Month) na Kampuni ya Emirate Aluminium Profile.
Bocco alitakiwa kukabidhiwa tuzo hiyo mwanzoni mwezi huu lakini kutokana majukumu ya Timu ya Taifa imebidi apewe leo.
Baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo Bocco amewashukuru wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliompa kwani peke yake asingeweza.
“Kwanza namshukuru Mungu kwa kunifikisha hapa pili nawashukuru wachezaji wenzangu kwa kunisasaidia hadi nimefanikiwa kushinda, naamini nitaendelea kufanya vizuri kwa kupata ushirikiano wao,” amesema Bocco.
Kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Emirate, Issa Maeda amewataka watu kuendelea kutumia bidhaa za kampuni hiyo huku akisisitiza waendelee kufanya kazi na Simba.
Kampuni ya Emirate imekuwa ikitoa kitita cha Sh 1,000,000 kwa mchezaji aliyepata kura nyingi zilizopigwa na mashabiki.
Bocco amepata asilimia 59 ya kura zilizopigwa mashabiki ndani ya mwezi Mei akiwashinda Bernard Morrison na Taddeo Lwanga alioingia nao fainali.
Mwezi uliopita Bocco alinyakua kitita cha Sh 2,500,000 kutoka Emirate baada ya kuibuka mchezaji bora wa mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Kaizer Chiefs.
2 Responses
Fantastic captain
congrats @John bocco 👏👏👏