Biriani la Derby laliwa Temeke

Kuelekea mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili katika Uwanja wa Benjamin Mkapa leo tumefanya hamasa pamoja na kujipongeza kwa kula biriani kutoka kwa Mwanahasa mwenzetu Fetete.

Biriani la leo ni maalum kabisa kwa ajili ya mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Yanga ambao tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunashinda.

Hamasa hiyo imeanzia Uwanja wa Benjamin Mkapa nakuzunguka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Temeke.

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema mchezo wa Derby umebeba taswira ya soka Tanzania hivyo mashabiki wanapaswa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuisaidia timu kupata ushindi ambao utawapa furaha.

“Mchezo wa Derby ya Kariakoo ndio kioo cha soka la Tanzania, furaha ya ushindi wake inadumu kuliko mechi yoyote hivyo Wanasimba kateni tiketi tukutaje Jumapili Benjamin Mkapa kuisaidia timu yetu kupata ushindi,” amesema Ahmed.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER