Benchikha: Tuna changamoto kwenye kumalizia nafasi

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema changamoto yetu kubwa iliyopo kwenye kikosi chetu ni kumalizia nafasi tunazotengeneza.

Benchikha amesema kila mchezo tunacheza vizuri na kumiliki sehemu kubwa lakini tunashindwa kuzitumia nafasi tunazozipata.

Benchikha ameongeza kuwa pamoja na kushindwa kupata ushindi katika mechi zilizopita lakini hatujakata tamaa kupambania ubingwa kwakuwa tumebakiwa na michezo 10.

“Kila mtu anajua, tunacheza vizuri tunatengeneza nafasi nyingi lakini tunashindwa kuzitumia na hilo ndilo tatizo kubwa.”

“Bado hatujakata tamaa kuendelea kupambania ubingwa kwakuwa, tukishinda mechi zote 10 zilizobaki tunakusanya alama 30 kwahiyo bado tuna nafasi ya kuchukua ubingwa,” amesema Benchikha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER