Benchikha: Tulistahili pointi tatu

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy uliopigwa Uwanja wa Obeid Ituni Chilume tulistahili kupata alama zote tatu.

Benchikha amesema tulicheza vizuri muda mwingi na kutengeneza nafasi lakini katika mita chache kutokana eneo la wapinzani Galaxy hatukuwa bora sana.

Benchikha ameongeza kuwa hajafurahishwa na matokeo ya sare kwakuwa anaamini kwa kiwango tulichoonyesha tulistahili kushinda.

“Sina furaha na matokeo haya ya sare, nadhani tulistahili ushindi kutokana na kiwango tulichoonyesha.

“Tumecheza vizuri karibia kila idara, shida ilikuwa katika eneo la tatu la wapinzani tulipoteza umakini uliotufanya kukosa nafasi nyingi,” amesema Benchikha.

Akizungumzia kundi letu jinsi lilivyo baada ya mechi mbili Benchikha amesema “kundi bado liko wazi timu yoyote ina nafasi ya kusonga mbele, sisi tunajipanga kwa ajili ya michezo yetu ijayo.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER