Benchikha: Mechi dhidi ya Wydad ni ya maamuzi kwetu

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amesema mchezo wa kesho dhidi ya Wydad Casablanca utaamua hatma yetu ya kutinga hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Benchikha amesema tunahitaji kupata pointi tatu kwenye mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na ubora walionao.

Hata hivyo Benchikha amesema anawaamini wachezaji wake na wapo kwenye hali nzuri kuhakikisha tunapata ushindi na kucheza soka safi.

“Kwetu ni mechi ya maamuzi. Tupo kamili kuhakikisha tunapata ushindi na kucheza soka safi, nawaamini wachezaji wangu wapo tayari kuhakisha ushindi unapatikana,” amesema Benchikha.

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ amesema mchezo wa kesho ni fainali kwetu ambao tunahitaji kushinda kwa kila namna ili kurejesha matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Zimbwe Jr ameongeza kuwa kila mchezaji yupo tayari kwa ajili mchezo huo na atapambana kuhakikisha Wanasimba wanapata furaha kwa kupata ushindi.

“Ni fainali kwetu, tunahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufanya vizuri, sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana hadi mwisho ili kupata ushindi,” amesema Zimbwe Jr.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER