Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha ameweka wazi kuwa hajaridhishwa na kiwango kilichoonyeshwa na kikosi chetu licha ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKU.
Benchikha amesema tumecheza vizuri lakini tulifanya makosa kadhaa hasa katika nafasi ya ulinzi ambayo yametufanya kuruhusu bao.
Benchikha amesema katika mashindano kama haya kufanya makosa hasa kwenye ulinzi ni hatari kwakuwa unakuwa kwenye nafasi ya kuruhusu kufungwa.
“Tumecheza vizuri nimefurahi kwa matokeo lakini sijaridhishwa na matokeo. Tumefanya makosa kadhaa kwenye nafasi ya ulinzi yaliyosababisha kuruhusu bao,” amesema Benchikha.
Benchikha ameongeza kuwa JKU ni timu nzuri na inacheza kwa mipango hasa katika eneo la kiungo.