Kocha Mkuu Abdelhak Benchikha amewapongeza wachezaji kwa kucheza soka safi licha ya kupata sare ugenini dhidi ya ASEC Mimosas katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Benchikha amesema ameridhishwa na jinsi timu ilivyocheza kwa umoja na kushirikiana na kusababisha kupatikana kwa pointi moja muhimu ugenini.
Benchikha ameongeza kuwa kwa sasa hakuna muda wa kupumzika maandalizi ya mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi dhidi ya Jwaneng Galaxy ambao utapigwa mwishoni wa juma lijalo yanaanza.
“Tunaushukuru Mungu kwa kutuwezesha kupata pointi moja ugenini, kama nilivyosema awali isingekuwa mechi rahisi lakini tumepambana hadi mwisho.
“Nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliyofanya sasa tunarejea nyumbani kwenda kujiandaa na mchezo wa mwisho dhidi ya Jwaneng,” amesema Benchikha.