Benchikha awamwagia sifa wachezaji ushindi dhidi ya Singida FG

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amewasifalu wachezaji kwa kuonyesha soka safi katika ushindi wa ambao 2-0 tuliopata dhidi ya Singida Fountain Gate katika mchezo wa Kombe la Mapinduzi uliopigwa Uwanja wa New Amaan Complex.

Benchikha amesema tulicheza vizuri kuanzia kwenye kuzuia hadi kushambulia na kuweza kumiliki sehemu kubwa ya mchezo.

Hata hivyo Benchikha ameisifu Singida Fountain Gate kwa kucheza soka la kasi pamoja na mashambulizi haraka ingawa tuliweza kuwamudu.

“Nawapongeza wachezaji wangu, tumecheza vizuri. Ilikuwa mechi ngumu yenye kasi lakini tulikuwa bora ndio maana tumeshinda.”

“Singida ni timu nzuri na inacheza soka la kushambulia na ilitupa upinzani mkubwa ingawa tulikuwa bora zaidi yao,” amesema Benchikha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER