Benchikha arejea, aongoza mazoezi ya mwisho

 

Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha amerejea nchini leo na jioni amekiongoza kikosi kwenye mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wetu wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mashujaa FC.

Benchikha alikwenda nchini Algeria kwa ajili ya kushiriki kozi fupi ya ukocha na tayari amerejea na kesho atakuwa kwenye benchi kukiongoza kikosi dhidi ya Mashujaa kwenye mchezo utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex saa 2:15 usiku.

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika jioni katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena wachezaji wote wameshiriki kikamilifu na wapo kwenye hali nzuri.

Tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-1 tuliopata juzi dhidi ya Singida Fountain Gate.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER