Mtendaji Mkuu wa klabu Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa tutarudisha mataji yote tuliyopoteza msimu uliopita kutokana na maandalizi tunayoendelea nayo.
Barbara amesema malengo yetu ni kurudisha ubingwa wa ligi ya NBC, Azam Sports Federation Cup na kufika Nusu Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Barbara ameongeza kuwa msimu huu hatuna kuteleza tena tumejipanga ndani na nje uwanja na hakutakuwa na jambo lakuturudisha nyuma.
“Safari hii hakuna kuteleza tena, tumejipanga kuhakikisha tunarudisha mataji yote kuanzia ligi kuu, FA na kufika Nusu Fainali ya Klabu Bingwa Afrika,” amesema Barbara.