Banda: Simba miongoni mwa timu tatu bora Afrika

Mchezaji mpya wa kimataifa wa Simba, Peter Banda, amesema kilichomfanya ajiunge na Wekundu wa Simba ni tamaa yake ya kuchezea mojawapo ya timu kubwa za Afrika.

Katika mazungumzo yake na Simba App jijini Dar es Salaam leo, Banda alisema anaamini kuna timu tatu kubwa barani Afrika kwa sasa – Al Ahly ya Misri, Mamelodi ya Afrika Kusini na Simba ya Tanzania.

“Nina ndoto kubwa za kucheza soka barani Ulaya lakini kama ni kubaki Afrika, basi nilitamani kucheza katika mojawapo ya timu kubwa za Afrika.

“Ukiniuliza mimi, kwa sasa, timu kubwa za soka hapa Afrika ni Simba, Al Ahly na Mamelodi Sundowns, alisema Banda ambaye juzi alitangazwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Malawi kinachojiwinda na Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2022.

Katika mazungumzo yake hayo ambayo video yake itaonyeshwa kwenye Simba App, Banda alisema alianza kusikia kuhusu Simba tangu angali na mdogo ingawa sasa ndiyo hasa amevutiwa kujiunga nayo.

Kabla ya kujiunga na Simba, Banda alikuwa akicheza nchini Moldova katika bara la Ulaya na ingawa uamuzi wake wa kurejea Afrika umewashtua Wamalawi wengi, anaamini amefanya uamuzi sahihi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER