Banda: Nilimuahidi mama nitafunga

Winga Peter Banda ameweka wazi kuwa alimuahidi mama yake atafunga katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas na amefanikiwa kutimiza ahadi yake.

Banda amesema kabla ya mchezo alimpigia simu mama yake kwa ajili ya kuomba baraka zake na mwisho wa maongezi alimwambia kuwa atafunga.

Nyota huyo raia wa Malawi amesema baada ya kufunga alishangilia na kuweka alama ya A vidoleni mwake akimaanisha herufi ya kwanza ya jina la mama yake yaanu Agnes.

Banda ameongeza kuwa kwa sasa malengo yake ni kuhakikisha anafanya vizuri katika kila mchezo atakaopangwa ili kuisaidia timu kupata matokeo.

“Kabla ya mechi nilimpigia simu mama kuomba baraka zake na nilimuahidi nitafunga na kweli nimefunga. Ndiyo maana nilishangilia kwa kuonyesha alama ya A ikiwa na maana Agnes.

“Malengo yangu ni kuhakikisha nafanya vizuri kwenye kila mchezo ili kuisaidia timu kupata pointi tatu kwenye mashindano yote,” amesema Banda.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER