Banda na mikakati ya AFCON

Nyota wetu Peter Banda, ambaye yuko katika timu yake ya taifa ya Malawi (The Flames) inayoshiriki Michuano ya AFCON nchini Cameroon amesema wanapaswa kuongeza jitihada ili kufanya vizuri katika mashindano hayo.

Banda ni mmoja ya wachezaji wa Malawi waliocheza vizuri dhidi ya Guinea jana ambapo alitumika nyuma ya washambuliaji wawili ili kuwa daraja la kutengeneza nafasi kwa The Flames.

Kwa dakika 80 alizokuwa uwanjani Banda alifanya kila jitihada kuisaidia Malawi kushinda lakini mchezo ulimalizika kwa Guinea kubeba pointi tatu kwa ushindi wa bao moja.

“Mchezo ulikuwa mzuri, nina furaha kuiwakilisha nchi yangu kwenye mashindano haya makubwa. Bado tuna mechi nyingi tunapaswa kuongeza jitihada ili kufanya vizuri,” amesema Banda.

Katika mchezo huo Banda alitengeneza nafasi mbili ambazo hazikutumiwa vizuri na wenzake huku akipiga mashuti mawili moja lililenga lango na lingine lilienda nje.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER