Banda arejea kikosini, aanza mazoezi Dubai

 

Winga wa kimataifa kutoka Malawi, Peter Banda ameanza mazoezi mepesi leo baada ya kukaa nje kwa takribani miezi miwili akiuguza jeraha la mguu.

Banda aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi Singida Big Stars uliopigwa Uwanja wa Liti, Novemba 9.

Banda amesafiri pamoja na kikosi jana kuelekea Dubai kwenye kambi ya mazoezi ya siku saba kujiandaa na mashindano mbalimbali yaliyo mbele yetu.

Kwenye mazoezi ya kwanza leo hii, Banda amefanya binafsi akiwa chini ya uangalizi wa madaktari.

Kwa mujibu wa Daktari wa Timu, Edwin Kagabo, Banda atafanya mazoezi hayo kwa siku tatu kabla ya kukabidhiwa kwa kocha wa viungo kwa ajili ya kurejesha utimamu wa mwili na kujiunga moja kwa moja na wenzake.

Naye Moses Phiri amejiunga na kikosi leo akitokea nyumbani kwao Zambia ambapo kuanzia kesho ataanza programu maalumu ya mazoezi.

Kurejea kwa Banda na Phiri ni furaha kwa Wanasimba katika nyakati hizi ambazo ligi imepamba moto na Michuano ya Ligi Mabingwa Afrika inakaribia kuanza mapema mwezi ujao.

Majeuruhi pekee ambaye amesalia ndani ya kikosi chetu ni Henock Inonga ambaye kwa sasa anauguza jeraha la kidonda baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER