Balozi wa Tanzania nchini Uganda awatia moyo wachezaji

Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mh. Dk. Aziz Ponary Mlima amewatia moyo wachezaji wetu kuwa tunaweza kupata pointi tatu katika mchezo wa kesho wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers.

Balozi Dk. Aziz amesema hayo alipowatembelea wachezaji kambini leo na kuongeza kuwa matumaini yake pamoja na Watanzania wote waishio Uganda ni kwamba kesho tutaibuka ushindi kutokana na ubora wa kikosi tulio nao.

Pamoja na mambo mengibe, Dk. Aziz ameenda mbali na kusema kesho tunaweza kupata ushindi wa mabao mawili na kuendelea kama wachezaji watatimiza majukumu yao uwanjani ipasavyo.

“Tunawatakia kila la heri, tena ushindi wa bao ambalo si moja au mbili bali matatu na kuendelea, lengo ni kushinda kwa maana hiyo mabalozi wa Tanzania tukiwa hapa sisi wote ni Watanzania.

“Matumaini yangu mtafika robo fainali kama kawaida yenu, tunaamini mechi ya kesho ni ya ushindi tutakuwa na furaha kuona mkiondoka na pointi zote tatu kesho,” amesema Dk. Aziz.

Dk. Aziz pia amewakumbusha wachezaji ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ya kutoa milioni tano kwa kila bao tutakalofunga hivyo amewaomba wachezaji kuhakikisha wanatumia fursa hiyo.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER