Baleke ni Mnyama

Uongozi wa Klabu ya Simba unatangaza kukamilisha usajili mshambuliaji wa kati Jean Othos Baleke raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo kwa mkataba wa miaka miwili kutoka TP Mazembe.

Baleke (21) anatarajia kuwasili nchini Jumanne na atajiunga na kikosi ambacho kitakuwa kimerejea kutokea Dubai.

Baleke amejiunga nasi akitokea Nejmeh FC ya Lebanon ambapo alipelekwa kwa mkopo mwanzoni mwa msimu huu.

Usajili wa Baleke ni matakwa ya benchi la ufundi ili kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji.

Baleke ni mchezaji wa tatu kusajiliwa kwenye dirisha hili akitanguliwa na Saido Ntibanzokiza na Ismael Sawadogo tuliyemtambulisha jana.

Kwa mujibu wa taratibu Baleke ataitumikia Simba kwenye mashindano yote ikiwemo Ligi ya mabingwa Afrika kwani hakucheza katika hatua za awali.

Wasifu wa mchezaji

Jina Kamili: Jean Toria Baleke Othos

Tarehe ya Kuzaliwa: Aprili 17, 2001

Umri: Miaka 21

Urefu: Mita 1,69

Uraia: DR Congo

Nafasi: Mshambuliaji wa kati

Klabu: Simba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER