Baleke, Chama, Manula wachuana mchezaji bora Machi

Nyota watatu Jean Baleke, Clatous Chama na mlinda mlango Aishi Manula wameingia fainali ya kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Machi (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Kabla ya kuchujwa na kubaki watatu awali walikuwa watano pamoja na viungo wakabaji Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin.

Katika mwezi Machi tumecheza mechi nne, moja Ligi Kuu ya NBC (Mtibwa Sugar), moja ya Azam Sports Federation Cup (African Sports) na mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika (Vipers, Horoya).

Takwimu za wachezaji wote za Machi

Dakika Magoli Assist

Baleke 271 6 1

Chama 273 4 1

Manula 270 sawa na mechi tatu akiwa hajaruhusu bao lolote.

Zoezi la kupiga kura kupitia kwenye tovuti yetu ya www.simba.co.tz limeanza leo na litafungwa Machi 31, saa sita usiku.

Mshindi atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

SHARE :
Facebook
Twitter

7 Responses

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER