Baleke apiga hat trick tukitinga Nusu Fainali ASFC Kibabe

Mshambuliaji Jean Baleke amefunga mabao matatu ‘hat trick’ katika ushindi wa 5-1 tuliyopata dhidi ya Ihefu FC katika mchezo wa Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Baleke alitupatia bao la kwanza dakika ya pili kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Clatous Chama.

Wakati Ihefu wanaendelea kujiuliza kwanini wameruhusu bao la mapema Baleke alitupatia la pili dakika ya 15 kwa shuti kali la mguu wa kushoto akimalizia pasi ya Kibu Denis.

Baleke alikamilisha ‘hat trick’ kwa kufunga bao la tatu dakika ya 28 baada ya mlinzi wa kulia Israel Patrick kuwapiga chenga walinzi wa Ihefu kabla ya kutoa pasi safi kwa mfungaji akiwa anatazamana na nyavu.

Saido Ntibazonkiza alitupatia bao la nne dakika ya 39 baada ya kumpoka mpira mlinzi wa kushoto wa Ihefu, Yahaya Mbegu na kupiga shuti kali la chini chini lililomshinda mlinda mpango Shaban Kado.

Raphael Daudi aliwapatia Ihefu bao lao pekee dakika ya 60 kwa kichwa akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Never Tigere.

Pape Sakho alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la tano dakika ya mwisho ya mchezo baada ya kupokea pasi ya Chama.

X1: Manula (Kakolanya 75′), Israel, Zimbwe Jr, Onyango (Mkude 61′) Henock (Kennedy 44′), Erasto, Chama, Mzamiru, Baleke (Mohamed 61′), Ntibazonkiza (Sakho 75′), Kibu.

Walioonyeshwa kadi: Israel 63′ Kibu 78′

X1: Kado (Masalanga 45), Mwaita, Mbegu, Nyoso, Kisu, Onditi, Tigere (Ngoah 68′), Loth, Simchimba (Yacouba 45′), Mahundi, Mwalyanzi (Rashidi 45′) (Adam 81′).

Walioonyeshwa kadi: Mahundi 8′ Rashidi Juma 54′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER