Baleke apiga hat trick tukiichapa Mtibwa Manungu

Mabao matatu ‘hat trick’ yaliyofungwa na mshambuliaji Jean Baleke yametosha kutupa ushindi wa 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Manungu Complex.

Baleke alitupatia bao la mapema dakika ya tatu akimalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Moses Phiri kabla ya kumzidi mjanja mlinzi wa Mtibwa.

Baleke aliongeza bao la pili kwa kichwa dakika ya saba baada ya kumalizia mpira uliopigwa na Saido Ntibanzonkiza kufuatia mpira wa kona aliyoanziwa na Clatous Chama.

Baleke alikamilisha hat trick kwa kutufungia bao la tatu dakika ya 33 kwa kichwa akimalizia mpira wa kichwa uliopigwa na Shomari Kapombe.

Hii ni hat trick ya kwanza kwa Baleke tangu ajiunge nasi katika dirisha dogo la usajili mwezi Desemba akiwa amefikisha mabao matano kwenye ligi.

Kipindi cha pili Mtibwa walirudi kwa kasi ambapo dakika 15 za mwanzo walifanya mashambulizi kadhaa ambayo hata hivyo yaliishia kwa walinzi wetu.

Ushindi wa leo umetufanya kufikisha pointi 57 tukiwa nafasi ya pili kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 24.

X1: Razak, Kajole, Issa, Kigi Mwihambi, Kotei (Chota 52′), Omary, Ganambali, Mayanga (Mpepo 58′) Chasambi (Mkele 69′), Kiziwa (Onesmo 52′)

Walionyeshwa kadi: Omary 64′ Mwihambi 79′

X1: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Henock (Kennedy 69′) Kanoute (Erasto 81′) Chama, Mzamiru, Baleke (Kyombo 81′) Ntibazonkiza (Banda 87′) Phiri (Mussa 81′)

Walionyeshwa kadi: Mzamiru 77′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER