Baleke apiga hat trick tukiichapa Coastal Uhuru

Mshambuliaji, Jean Baleke amefunga hat trick katika ushindi wa 3-0 tuliopata dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Baleke alitupatia bao la kwanza dakika ya sita baada ya kumalizia pasi safi ya Clatous Chama akiwa ndani ya 18.

Dakika ya 10 Baleke alitupatia bao la pili baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi wa kushoto Mohamed Hussein.

Winga Hijja Ugando alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 20 baada ya kumuumiza Henock Inonga ambaye alishindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikachukuliwa na Kennedy Juma.

Baleke alikamilisha hat trick kwa kufunga bao la tatu dakika ya 40 kwa mkwaju wa penati baada ya Luis Miquissone kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Ushindi huu unatufanya kuifikisha alama tisa baada ya kushinda mechi zote za tatu za ligi.

X1: Lakred, Kapombe (Israel 72′), Zimbwe Jr, Che Malone, Henock (Kennedy 20′), Mzamiru (Kanoute 72′), Chama, Ngoma, Baleke (Kibu 72′), Ntibazonkiza (Onana 79′), Miquissone

Walioonyeshwa kadi: Che Malone 45+1, Kanoute 76′

X1:Chuma, Cosmas, Miraji, Lameck, Daud, Semfuko, Ugando, Gwalala, Bakari, Ajibu, Dennis

Walioonyeshwa kadi: Gwalala 13′ Ugando (nyekundu 20′) Cosmas 28′ Chuma 87′

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER