Baleke amfikia Bocco kwa Hat trick

Mshambuliaji Jean Baleke ameifikia rekodi ya nahodha John Bocco kwa kufunga mara mbili mabao matatu kwenye mechi moja ‘hat trick’ msimu huu.

Katika ushindi wa 5-1 tuliyopata katika mchezo wa Robo Fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Ihefu FC, Baleke amefunga matatu ‘hat trick’s.

Machi 11, Baleke alifunga mabao matatu katika ushindi 3-0 tuliupata katika Uwanja wa Manungu, Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar.

Nahodha John Bocco alikuwa ndiye pekee aliyekuwa amefunga mabao matatu katika mechi mbili msimu huu kabla ya Baleke kumfikia.

Nyota wengine waliofunga hat trick kwenye kikosi chetu ni Moses Phiri, Saidi Ntibanzonkiza na Clatous Chama.

Hizi ndizo hat trick tulizofunga mpaka sasa……

John Bocco ( Simba 4-0 Ruvu Shooting) Novemba 11, 2022 Ligi Kuu ya NBC

Moses Phiri (Simba 8-0 The Eagle) Desemba 10, 2022, Azam Sports Federation Cup.

John Bocco (Simba 7-1 Tanzania Prisons) Desemba 30, Ligi Kuu ya NBC.

Saidi Ntibazonkiza (Simba 7-1 Tanzania Prisons) Desemba 30, Ligi Kuu ya NBC.

Jean Baleke (Mtibwa 0-3 Simba) Machi 11, 2023, Ligi Kuu ya NBC.

Clatous Chama (Simba 7-1 Horoya) Machi 18, 2023 Ligi ya Mabingwa Afrika.

Jean Baleke (Simba 5-1 Ihefu) Aprili 7, 2023 Azam Sports Federation Cup.

Hii ina maana tumefunga hat trick kwenye michuano yote tuliyoshiriki msimu huu ambapo jumla yake ni saba.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER