Baleke alezea furaha ya kupiga hat trick

Mshambuliaji Jean Baleke ameweka wazi kuwa amefurahi kufunga mabao matatu ‘hat trick’ kwa mara ya kwanza akiwa na kikosi chetu.

Baleke amefunga hat trick hiyo katika ushindi wa mabao 3-0 tuliopata leo dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa Uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro.

Baleke amesema ni furaha kwa kila mshambuliaji kufunga na kuisaidia timu kupata ushindi umuhimu.

Baleke ameahidi kuendelea kuonyesha umwamba wa kufumania nyavu kila atakapopata nafasi ya kufanya hivyo.

“Nina furaha kufunga hat trick ya kwanza nikiwa na Simba. Mimi ni mshambuliaji kazi yangu ni kufunga kwahiyo nawaahidi nitaendelea kufunga,” amesema Baleke.

Baleke amefunga mabao hayo katika kipindi cha kwanza kwenye dakika za tatu, saba na 33.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER